• July 16, 2026
  • Mwandishi Wetu
  • 0

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na wachezaji saba kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2026/27.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, klabu hiyo imewashukuru wachezaji hao kwa mchango wao ndani ya timu na kuwatakia kila la heri katika hatua zao zinazofuata za maisha ya soka.

Wachezaji walioachwa na Simba SC ni:
πŸ‘‹ Chamou Karaboue
πŸ‘‹ Naby Camara
πŸ‘‹ Edwin Balua
πŸ‘‹ Joshua Mutale
πŸ‘‹ Awesu Awesu
πŸ‘‹ Omari Omari
πŸ‘‹ Moussa Camara

Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya kikosi yanayofanywa na Simba SC kuelekea msimu mpya, huku mashabiki wakisubiri kuona wachezaji watakaojiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *