Bweni la wanafunzi wa kiume katika Shule ya Sekondari ya Kalangalala, mkoani Geita, limenusurika kuteketea kwa moto baada ya kuzuka kwa moto ndani ya bweni hilo katika tukio lililosababisha taharuki miongoni mwa wanafunzi, walimu na wananchi.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Kenneth Mwakasitu, tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita na dakika 16 mchana. Amesema moto huo uliweza kuzimwa mapema na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu, jambo alilosema limetokana na elimu ya kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto ambayo Jeshi la Zimamoto limekuwa likiitoa mashuleni.



























