Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kushirikiana na Benki ya Azania, imezindua rasmi mpango wa utoaji wa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo utakaowezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vidogo vya kuuza mafuta ya petroli na dizeli katika maeneo ya vijijini.



























