Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuwa walinzi wa mali za umma, akieleza kuwa mtu anayeharibu miundombinu hiyo, anateketeza kodi za wananchi.
Samia amefafanua kuwa fedha inayokusanywa na Serikali, kisha kutolewa kama mchango katika utekelezaji wa miradi, hizo ni kodi za wananchi, hivyo hawatakubali ziteketezwe kiuhalisi.
Dk Samia ameeleza hayo leo Agosti 7,2026 wakati akifungua na kutembelea Mradi wa Mabasi Yanayoenda Haraka Awamu ya Pili (BRT II) katika barabara ya Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa jijini Dar es Salaam.



























