• July 21, 2026
  • Mwandishi Wetu
  • 0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Tanzania inaendelea kukabiliwa na vitisho vinavyofanana na vile vilivyowaleta wakoloni barani Afrika, akieleza kuwa safari hii vinakuja kwa mbinu tofauti.

Katambi ametoa kauli hiyo leo wilayani Karatu, mkoani Arusha, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania, ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *