Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ni eneo lenye historia ya kipekee katika ujenzi wa taifa kutokana na mchango wake wa kuzalisha viongozi wakubwa wa nchi na kuwa kitovu cha mafunzo ya maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Lowassa-Sepeko wilayani Monduli, Chongolo amesema Monduli imeendelea kuwa alama ya uzalendo na uongozi, akibainisha kuwa karibu kila afisa wa jeshi nchini amepitia mafunzo katika eneo hilo.




























