Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 Jaji Shabani Lila amesema tume hiyo imeanza kazi ya kukutana na wananchi na wameanza na Mkoa wa Dar es salaam katika Wilaya ya Kigamboni.
Jaji Lila amewataka wananchi wa Kigamboni kujitokeza kwa wingi kuanzia leo tarehe 24 na tarehe 26 kwa ajili ya kutoa shuhuda zao huku akisisitiza usiri na usalama wa mashuhuda.





























































































































































































































































