Maafisa na askari wanaoshiriki mafunzo ya Shirikisho la Kimataifa la Askari wa Kike na Wasimamizi wa Sheria (IAWP) nchini Indonesia, wameeleza kuwa mafunzo ya siku ya leo yamewapa fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za kiutendaji pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea.
Washiriki hao wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa na maarifa katika nyanja mbalimbali za kiutendaji, huku wakibainisha kuwa kila mmoja anatarajia kutumia maarifa na uzoefu walioupata katika kuboresha utendaji katika maeneo yao ya kazi nchini Tanzania.
Aidha, wamesema kubadilishana uzoefu na maafisa kutoka mataifa mbalimbali kumewapa fursa ya kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na changamoto za kiutendaji, pamoja na kuona namna nchi nyingine zinavyotekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Wameahidi kuhakikisha kuwa maarifa na uzoefu wanaoupata kupitia mafunzo hayo yanatumika kuleta maboresho katika utendaji wao wanaporejea katika maeneo yao ya kazi.





























































































































































































































































