Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Asha Mbaruk kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akichukua nafasi ya Dk. Ayub Chacha ambaye amemaliza muda wake.
Kabla ya uteuzi huo, Mbaruk alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).





























































































































































































































































